Thursday, June 21, 2018

JIJI ‘LAMWAGA’ MAMILIONI KWA VIJANA, WANAWAKEKaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Dodoma Mufungo Manyama akizungumza na viongozi wa vikundi 137 vya Wanawake na Vijana wakati wa semina elekezi kwa viongozi hao kuhusu uendeshaji wa vikundi na matumizi ya fedha za mikopo kabla ya kupatiwa mkopo wa milioni 344 mapema wiki ijayo.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Dodoma Mufungo Manyama akizungumza na viongozi wa vikundi 137 vya Wanawake na Vijana wakati wa semina elekezi kwa viongozi hao kuhusu uendeshaji wa vikundi na matumizi ya fedha za mikopo kabla ya kupatiwa mkopo wa milioni 344 mapema wiki ijayo.

.....................................................
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inatarajia kutoa takribani shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya Wajasiriamali Wanawake na Vijana kwa mwaka wa fedha unaomalizika Mwezi Juni, 2018.

Jumla ya vikundi 137 vinatarajiwa kunufaika na fedha hizo zinazotokana na makusanyo ya kodi za ndani ya Halmashauri (Own Source) ambapo  vikundi vya Wanawake ni 102 na vya vijana 37.

Akizungumza wakati akitoa semina elekezi kwa viongozi wa vikundi hivyo katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma leo Juni 21, 2018, Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Dodoma Mufungo Manyama aliwaeleza wajumbe kuwa awamu ya mwisho ya mikopo kwa mwaka huu wa fedha itatolewa katikati ya wiki ijayo ambapo jumla ya Shilingi milioni 344 zitakabidhiwa kwa vikundi hivyo.

Aliwataka Wanavikundi hao kuwa makini na matumizi ya fedha wanazokopeshwa na kufanya marejesho kwa wakati ili wapate fursa ya kukopeshwa zaidi.

Kwa upande wao, baadhi ya viongozi wa vikundi hivyo waliishukuru Halmshauri ya Jiji na kuahidi kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili waweze kurejesha kwa wakati hali itakayopelekea kunufaisha vikundi vingi zaidi.No comments:

Post a Comment