Monday, September 18, 2017
Wednesday, September 6, 2017
Monday, September 4, 2017
ARDHI YOTE MANISPAA YA DODOMA KUPIMWA NDANI YA MIAKA MIWILI
..................................................................
Mpango huo umewekwa
wazi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi alipozungumza na
waandishi wa Habari katika ukumbi wa Manispaa juzi.
Alisema miradi ya
upimaji wa ardhi katika utekelezwaji wa lengo hilo haitafanywa na Manispaa
pekee bali itashirikisha taasisi
mbalimbali zenye uzoefu wa miradi ya aina hiyo.
Alifafanua kuwa, mbali
na kushirikisha taasisi za Umma na binafsi, Manispaa ya Dodoma ina mkakati wake
wa upimaji na tayari baadhi ya Kata zimeshaanza kupimwa ambapo pia, upo mkakati
wa kuongeza nguvu kazi kwa upande wa watumishi kwa kuajiri wataalamu wa ardhi
kwa mikataba ya muda ili kufikia lengo lililowekwa kwa wakati.
Manispaa ya Dodoma
inaundwa na Kata 41, ambapo ina jumla ya eneo la mraba 2,769, ambapo zaidi ya
nusu ya eneo hilo bado halijapimwa.
Monday, August 21, 2017
MEYA WA MANISPAA YA DODOMA PROF DAVIS MWAMFUPE ATOA SOMO MAONESHO YA NANENANE
HALMASHAURI
za Manispaa na Wilaya katika mikoa ya Kanda ya Kati unayoundwa na mikoa ya Dodoma na Singida kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wanaounga mkono shughuli za kilimo, mifugo na
uvuvi wameshauriwa kubuni njia rahisi inayoweza kuwafikishia kwa wakulima na wafugaji elimu
inayopatikana kwenye viwanja vya Maonesho ya Wakulima maarufu kama Nanenane.
Rai hiyo
imetolewa na Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe kufuatia maenesho ya Nanenane yaliyomalizika
hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo amesema bado Maonesho hayo hususan Kanda ya Kati hayajafanikiwa
kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi wetu kwa kiasi kinachoridhisha na
kuwawezesha kubadili shughuli zao na kuzifanya kuwa na tija inayoridhisha.
Alisema
Maonesho ya Nane Nane yamekuwepo kwa miaka mingi katika Kanda mbalimbali nchini
na yamekuwa na mambo ya kuvutia sana hususani Teknolojia na mbinu bora za
uzalishaji katika kilimo na mifugo ambazo zinauwezo wa kuleta tija kubwa lakini
bado changamoto kubwa ni kwamba mambo yote bora na mazuri yanayopatikana kwenye
Maonesho hayajaweza kumfikia mkulima kwenye ngazi za msingi kwa maana ya ngazi
ya kaya na vijiji.
Alisema
kuwa, unaweza kutoka umbali usiozidi kilomita mbili tu kutoka kituo (Uwanja)
cha Maonesho kilipo utashangaa kukuta mkulima analima kilimo cha kienyeji
ambacho hakina manufaa.
“Teknolojia inayooneshwa kwenye Maonesho haya bado haijaweza kuwafikia
wakulima na wafugaji wetu kwenye vijiji vyao wanakoendesha shughuli zao za
kilimo na mifugo” alisema Profesa Mwamfupe na kuongeza kuwa, bado teknolojia na
ubunifu unaopatikana kwenye Maonesho haya unahitaji kuwafikia wakulima wa chini
kabisa.
Alitoa
wito kwa Mamlaka zinazohusika kuhakikisha Kiwanja cha Maonesho ya Nane Nane
Kanda ya Kati kilichopo katika Kata ya Nzuguni Manispaa ya Dodoma kinakuwa kituo cha Shamba Darasa la kilimo
mifugo na uvuvi cha kudumu ili wataalamu
wa kilimo na mifugo wawepo kituoni hapo kipindi chote cha mwaka wakisimamia shughuli
za kilimo na mifugo kituoni hapo na Halmashauri zilete Wakulima na Wafugaji wao
kujifunza na kupata suluhisho la changamoto zinazowakabili katika shughuli zao
za uzalishaji.
Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe (wa kwanza kulia) akishuhudia mmoja ya banda la maonesho alipotembelea Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati katika Viwanja vya Nzuguni Manispaa ya Dodoma hivi karibuni.
Thursday, August 17, 2017
MANISPAA YA DODOMA YATENGA ENEO MAALUM LA MACHINGA
........................................................................................
HALMASHAURI ya Manispaa
ya Dodoma imetenga eneo la Makole D-Center lililoko katikati ya Mji wa Dodoma kuwa
eneo rasmi kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo maarufu kama Machinga kufanya
biashara zao badala ya kupaga bidhaa ovyo mitaani hali inayopelekea kuharibu
taswira ya mji.
Hatua hiyo pia
itasaidia kuendana na kasi kubwa ya ongezeko la wafanyabiashara hao kuingia
Mjini humo kutoka mikoa mbalimbali nchini tangu Serikali ilipohamia rasmi Dodoma
ambako ni Makao Makuu ya Nchi.
Akizugumza katika
mkutano wa Baraza la Madiwani la kufunga wa fedha uliopita lililofanyika
mwishoni mwa wiki iliyopita katika
ukumbi wa Manispaa hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin aliyewajulisha
wajumbe na wananchi kuwa, sasa Manispaa iko katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi
wa miundombinu muhimu katika eneo hilo ikiwemo
vyoo ili shughuli za biashara zifanyike katika mazingira salama na rafiki.
“Tunatarajia eneo hilo
litakuwa tayari kufikia mwisho wa mwezi Agosti au mwanzo wa mwezi Septemba
mwaka huu mara moja tutaanza zoezi la kuwahamishia wafanyabiashara hao pale”
alifafanua.
Alisema Manispaa inashirikiana
kwa karibu na viongozi wa wafanyabiashara hao katika zoezi hilo, na kwamba
endapo eneo hilo halitatosha, wafanyabiashara wengine watahamishiwa katika eneo
la Chaduru .
Tayari Manispaa ya
Dodoma ilishaanza zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wa Matunda na chakula
katika maeneo yasiyo rasmi na kuwahamishia katika maeneo rasmi ya masoko
ikiwemo soko la Sabasaba, Bonanza, na Tambukareli.
Thursday, August 10, 2017
NAIBU MEYA WA MANISPAA YA DODOMA JUMANNE NGEDE ATETEA NAFASI YAKE
| Mgombea aliyeshindwa nafasi ya Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Samwel Mziba (CHADEMA) akitoa neno kwa wajumbe mara baada ya matokeo kutangazwa kufuatia uchaguzi uliofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa hiyo. |
...............................................................................................
..............................................................
NAIBU
Meya wa Manispaa ya Dodoma aliyemaliza muda wake Jumanne Ngede amefanikiwa
kutetea nafasi yake katika uchaguzi uliofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa
ya Dodoma ambapo wajumbe 56 walishiriki uchaguzi huo.
Katika uchaguzi huo
Ngede ambaye ni Diwani wa Kata ya Chamwino kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 47 dhidi ya mpinzani wake kutoka Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Samwel Mziba ambaye ni Diwani wa Kata ya Hazina aliyepata
kura 9.
Mkurugenzi wa Manispaa
ya Dodoma ambaye ni Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Dodoma Mjini Godwin
Kunambi alimtangaza rasmi Ngede kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Dodoma.
Baada ya kufanikiwa
kutetea nafasi yake, Ngede aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua kwa kura nyingi
jambo linaonesha kuwa wana imani kubwa na utendaji wake na kwamba ataendelea
kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kwa kushirikiana na Madiwani wote.
Kwa upande wake, mgombea
aliyeshindwa Samweli Mziba aliwashukuru wajumbe na kumpongeza mshindi huku
akidai uchaguzi umepita na sasa ni kuchapa kazi tu.
Monday, July 31, 2017
WANAOVAMIA MAENEO, UJENZI HOLELA MANISPAA YA DODOMA SIKU ZAO ZINAHESABIKA
.................................................................................................
MKURUGENZI wa Manispaa
ya Dodoma Godwin Kunambi ametoa wito kwa wakazi wa Manispaa hiyo kuacha mara
moja uvamizi wa maeneo ya wazi na yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi za misitu
ambapo watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha amewataka
wanaojenga nyumba za makazi au za biashara katika maeneo yasiyo rasmi na ambayo
hayakupimwa kusitisha shughuli za ujenzi na kubomoa majengo hayo kwa hiyari yao
vinginevyo Halmashauri ya Manispaa itayabomoa.
Alisema hayo jana wakati
akizungumza wa wamiliki wa nyumba za kupanga na Maofisa Watendaji wa Kata wa
Manispaa ya Dodoma katika ukumbi wa Dodoma Sekondari, ambapo alisema kujenga
katika maeneo yasiyopimwa ni kinyume na sheria na Manispaa ya Dodoma imejipanga
kusimamia hilo kikamilifu.
Alisema Manispaa ya
Dodoma imejipanga kuanza upimaji wa viwanja kwa kasi ili kuwawezesha wananchi hususan wakazi wa Dodoma kujenga kwa
kuzingatia sheria za Mipango Miji na kwamba upimaji huo utaenda sambamba na
utoaji wa vibali vya ujenzi katika kipindi kisichozi siku saba kwa mmiliki wa
kiwanja.
Kwa upande wa wamiliki
wa nyumba za kupanga, aliwataka kuungana na kuwa na umoja na uongozi wao ili
kuepukana na madalali ambao baadhi yao sio waaminifu, huku akiwapa changamoto
ya kujenga nyumba zaidi za makazi na kuziimarisha zilizopo huku akiwajulisha
kuwa, hivi karibuni watumishi wa
Serikali zaidi ya 2,000 wanatarajiwa kuhamia Mjini Dodoma ikiwa ni awamu ya
pili ya Serikali kuhamia Dodoma hivyo mahitaji ya nyumba za kuishi yatakuwa
makubwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)



