Tuesday, February 13, 2018

WANANCHI WAUNGA MKONO BOMOA BOMOA, WANAOHAMIA DODOMA WATAHADHARISHWA


Zoezi la ubomoaji lililoendeshwa na Manispaa ya Dodoma likiwa limeanza mapema jana asubuhi katika baa maarufu Mjini Dodoma ya Chako ni Chako baada ya Mmiliki wake kudaiwa kukiuka masharti ya kibali chake cha ujenzi.
Zoezi la ubomoaji lililoendeshwa na Manispaa ya Dodoma likiwa linaendelea mapema jana asubuhi katika baa maarufu Mjini Dodoma ya Chako ni Chako baada ya Mmiliki wake kudaiwa kukiuka masharti ya kibali chake cha ujenzi.
Zoezi la ubomoaji lililoendeshwa na Manispaa ya Dodoma likiwa linaendelea mapema jana asubuhi katika baa maarufu Mjini Dodoma ya Chako ni Chako baada ya Mmiliki wake kudaiwa kukiuka masharti ya kibali chake cha ujenzi.
Sehemu ya Baa Tango iliyopo eneo la Uhindini katikati ya Mji wa Dodoma nayo ilikumbwa na Bomoa Bomoa iliyoendeshwa na Manispaa ya Dodoma baada ya mmiliki wake kukiuka taratibu za ujenzi.
Sehemu ya Baa Tango iliyopo eneo la Uhindini katikati ya Mji wa Dodoma nayo ilikumbwa na Bomoa Bomoa iliyoendeshwa na Manispaa ya Dodoma baada ya mmiliki wake kukiuka taratibu za ujenzi.
Baadhi ya wasimamizi wa zoezi la bomoa bomoa (kulia) wakisaidia kutoa nje vifaa vya wapangaji wa nyumba iliyojengwa kwa kukiuka taratibu za ujenzi katika eneo la Kisasa jana kabla ya nyumba hiyo kubolewa wakati wa zoezi lililoendeshwa na Manispaa ya Dodoma.
Ubomoaji wa vibanda vilivyojengwa kando ya Barabara kuu ya Dodoma-Dar es Salaam ukiendelea wakati wa zoezi lililoendeshwa na Manispaa ya Dodoma jana.
Afisa Mdhibiti wa Ujenzi wa Manispaa ya Dodoma Ally Bellah akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari juu ya zoezi la bomoa bomoa lililoendeshwa na Manispaa ya Dodoma jana.

.....................................

BAADHI ya Wakazi wa Manispaa ya Dodoma wameunga mkono zoezi la kubomoa nyumba na vibanda vilivyojengwa katika maeneo ya yasiyo rasmi ikiwemo hifadhi za barabara, maeneo ya wazi, na wale waliojenga katika viwanja wasivyovimiliki linalofanywa na Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.

Baadhi ya wananchi waliotoa maoni yao katika maeneo ya Kisasa, Majengo, Nkuhungu, na Kikuyu ambapo zoezi hilo lilitekelezwa hapo jana, wamesema kumekuwapo na mazoea ya watu kuvamia maeneo yasiyo rasmi na kuanzisha makazi au vibanda vya biashara japo linaloharibu taswira ya Mji.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la siku mbili lililoanza jana, Afisa Mdhibiti Ujenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Ally Bellah alisema zoezi hilo linafanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba taratibu zote zimefuatwa kabla ya kufikia hatua ya uvunjaji.
“Maeneo yote haya tunayovunja wahusika walishapewa notisi kwa mujibu wa Sheria lakini wengi wao wamekaidi…kwa wale waliostahili kupewa fidia walishapewa fidia zao muda mrefu” alisema.
Bellah ametoa wito kwa Wakazi wote wa Manispaa ya hata wageni wanaohamia kuepuka kununua ardhi kienyeji kwani wanaweza kutapeliwa na kuuziwa maeneo ya wazi au yasiyo ya makazi na kujikuta wakipata usumbufu usio wa lazima.

“Hata wageni wanaohamia Manispaa ya Dodoma niseme kwamba tunawapenda sana na tunawakaribisha ila watakapohitaji ardhi au viwanja kwa ajili ya kujenga wahakikishe wanawasiliana na Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ili wawe salama” alisistiza
Alisema Mji wa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi hivyo lazima uwe na muonekano wa kuvutia na kwamba zoezi la bomoa bomoa ni endelevu ili kudhibiti ujenzi holela na kusimamia ujenzi bora kwa mujibu wa vibali vinavyotolewa.
      

No comments:

Post a Comment