Thursday, February 1, 2018

UJENZI WA STENDI KUBWA YA KISASA DODOMA KUANZA MACHI, NI YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana Mjini hapa jana. Wa pili kushoto ni Meya wa Manispaa hiyo Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe akiteta jambo na Naibu Meya Jumanne Ngede. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia Mkutano wa Baraza hilo jana.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika jana Mjini hapa jana.
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Wageni waalikwa wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani la  Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia Mkutano wa Baraza hilo jana.
...................................................................

UJENZI wa stendi ya mabasi kubwa na ya kisasa  katika Manispaa ya Dodoma unatarajiwa kuanza mapema mwezi Machi mwaka huu katika eneo la Nzuguni nje kidogo ya Mji wa Dodoma.

Jumla ekari 50 zimetengwa katika eneo hilo lililopo mashariki mwa Mji barabra ya Dodoma-Dar es Salaam, ambapo ujenzi wa stendi hiyo unatarajiwa kukamilika baada ya kipindi cha miei 24.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika Mjini hapa kwa ajili ya kupokea taarifa mbalimbali za kimaendeleo zilizotekelezwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa Fedha 2018/2019 kinachoanzia Mwezi Septemba hadi Desemba 2018.


Kunambi aliwaambia wajumbe wa Mkutano huo kuwa, stendi hiyo ni kubwa na ya kisasa yenye hadhi ya Makao Makuu ya Nchi, na kwamba itakuwa ya mfano kwa Nchi zote za ukanda wa afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment