Thursday, December 21, 2017
Wednesday, December 20, 2017
RC ATEMBELEA DAMPO LA KISASA MANISPAA YA DODOMA, ASEMA DODOMA LAZIMA IWE SAFI ZAIDI
| Sehemu ya pili ya Dampo la kisasa la Chidaya katika Manispaa ya Dodoma linalotumia Teknolojia ya kuzika taka ardhini ambayo bado haijaanza kutumika kwa sasa. |
.........................................................
MKUU wa Mkoa wa Dodoma
Dokta Binilith Mahenge amesema Mji wa Dodoma hauna sababu ya kuwa mchafu kwa
sababu Manispaa ya Dodoma imetekeleza mradi wa ujenzi wa dampo la kisasa na
litakalodumu kwa miaka mingi ijayo.
Aliyasema hayo baada ya kutembelea dampo la
kisasa la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma lililopo eneo la Chidaya Kata ya
Matumbulu takribani umbali wa kilometa 12 kutoka katikati ya Mji wa Dodoma.
Katika ziara hiyo fupi,
Mkuu huyo wa Mkoa alioongozana na Katibu Tawala wa Mkoa huo Rehema Madenge
pamoja na Mkuu wa Idara ya Mazingira na Usafishaji wa Manispaa hiyo Dickson
Kimaro aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi.
Awali mara baada ya
kuwasili katika eneo la dampo, Mheshimiwa Mahenge alielezwa jinsi Dampo hilo la
kisasa linavyofanya kazi na Mhandisi wa Mazingira wa Manispaa ya Dodoma
Barnabas Faida, aliyemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa, dampo hilo linatumia teknolojia
ya kuzika taka ardhini (Sanitary Landfill) ambayo ni rafiki kwa mazingira na afya
za wakazi wa maeneo ya karibu na dampo.
Mhandisi Faida alimjulisha
Mheshimiwa Mahenge kuwa, dampo hilo tayari limeanza kufanya kazi mapema mwaka
huu, na limejengwa kwa fedha za mradi wa Kuimarisha Miji ya Kimkakati Tanzania (TSCP)
unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na kuratibiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
Monday, December 18, 2017
WAKAZI WA MTAA DODOMA WALAMBA MILIONI 1 KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MTAA WAO
| Zoezi la usafi likiendelea katika Mtaa za Zahanati Kata ya Kikuyu Kaskazini Manispaa ya Dodoma. |
...............................................
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dokta
Binilith Mahenge ameahidi kutoa motisha ya Shilingi 1,000,000 kwa wakazi wa
mtaa wa Zahati uliopo Kata ya Kikuyu Kaskazini katika Manispaa ya Dodoma
kufuatia wakazi hao kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi wa Mazingira unaofanyika
kila Jumamosi katika Manispaa hiyo.
Mheshimiwa Mahenge alitoa
ahadi hiyo wakati alipowaongoza wakazi hao katika zoezi la usafi wa Mazingira
katika Mtaa huo mwishoni mwa wiki, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kufanya usafi
wa Mazingira kila Jumamosi aliyoianzisha yeye mara tu baada ya kuhamishiwa Mkoa
humo, kwa lengo la kuuweka Mji Mkuu wa Nchi katika hali ya usafi wakati wote.
Alisema fedha atakazowapa
wakazi wa Mtaa huo ni motisha na kuwaunga mkono kwa juhudi walizoonesha na
kwamba zitawasaidia katika kuboresha hali ya usafi katika eneo lao kwa kununua
vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi.
Alisema amefurahishwa na
namna wakazi wa Mtaa wa Zahati walivyojitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo
na kutoa wito kwa wakazi wa maeneo mengine katika Manispaa kuiga mfano huo ili
kwa pamoja waweze kuufanya Mji wa Dodoma kuwa namba moja kwa usafi wa Mazingira
nchini.
Wednesday, December 13, 2017
KAMPENI YA USAFI DODOMA: ABIRIA WALIPONZA BASI LA IMMO EXPRESS NA SPIDER,YAKUMBANA NA RUNGU LA MANISPAA
..................................
HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma imeendelea kuwakumbusha wakazi wa Manispaa kuendelea kuzingatia suala la usafi wa Mazingira na kutotupa taka ovyo katika lolote ndani Manispaa hiyo kwani atakayefaya hivyo atapambana na mkono wa sheria ikiwemo kulipa faini inayoanzia shilingi 50,000 hadi 300,000 au kutumikia kifungo cha miezi sita jela.
Rai hiyo pia inawahusu wasafiri wote wanaoingia Mjini Dodoma au kupitia wakielekea mikoa mingine kwamba wajiepusha kutupa uchafu ovyo nje ya vyombo vyao vya usafiri ikiwemo mabaki ya vyakula kwani wakibainika watachuliwa hatua za kisheria kama wachafuzi wengine.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Mazingira na Usafishaji wa Halmashauri hiyo Dickson Kimaro jana wakati alipowaongoza askari Jamii wa Manispaa hiyo kukamata mabasi ya Kampuni ya Immo Express na Spider baada ya baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri na mabasi hayo kudaiwa kutupa uchafu katika eneo la Nala barabara kuu ya Dodoma-Singida, ikiwemo mifuko ya plastiki iliyokuwa na mabaki ya vyakula.
Kufuatia tukio hilo, mabasi hayo yalitozwa faini ya Shilingi 50,000 kwa kila kampuni na baada ya kulipa yaliachiwa na kuendelea na safari.
Manispaa ya Dodoma imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha Mji Mkuu wa Nchi unakuwa safi muda wote, ambapo hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dokta Binilith Mahenge alitangaza Kampeni ya Usafi wa Mazingira mjini humo ambapo sasa usafi utafanyika Jumamosi ya kila wiki.
Katika utaratibu huo, Wananchi wote wanatakiwa kufanya usafi katika maeneo yao ya makazi, maeneo ya biashara, na maeneo ya wazi.
Tuesday, December 12, 2017
MANISPAA YA DODOMA YATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI KUANGAMIZA MAZALIA YA MBU WAENEZAO MALARIA
Friday, December 8, 2017
WALIOVUNJIWA VIBANDA KWENYE HIFADHI YA RELI DODOMA WAPATIWA ENEO NA MANISPAA
..............................................
HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma inatarajia kuwapatia eneo wafanyabiashara zaidi ya 550 waliovunjiwa vibanda vyao na kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) katika stendi ya mabasi madogo ya Jamatini ili kupisha utekelezaji wa mradi wa Reli ya kisasa, ili waendelee kufanya biashara zao kama kawaida.
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amewaeleza wafanyabiashara hao
kuwa, Manispaa iko katika hatua za mwisho kuandaa eneo la Makole D-Center kwa
kuweka miundombinu muhimu ikiwemo mfumo wa maji safi na maji taka ili
wafanyabiashara hao waanze kufanya shughuli zao mara moja na katika mazingira
rafiki na salama katika eneo hilo.
Aliyasema hayo
alipotembelea eneo la Jamatini na Stendi Kuu Novemba 6 mwaka huu, akiambatana
na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma, pamoja na Naibu Meya wa Halmashauri ya
Manispaa hiyo Jumanne Ngede kwa lengo la kuwapa pole wafanyabiashara hao na
kuwajulisha hatua zilizochukuliwa na Viongozi mbalimbali katika kuhakikisha
tatizo linalowakabili linapatiwa ufumbuzi kwa wakati.
Aliwatoa hofu ya kuwa eneo hilo halitakuwa na
wateja wengi kama ilivyokuwa eneo la stendi ya Jamatini, ambapo aliwaambia
tayari Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Daktari Binilith Mahenge ametoa maelekezo kwa
Manispaa na Sumatra kuhakikisha daladala zinakuwa na ruti inayopita katika eneo
hilo jipya la biashara ambapo abiria watakuwa na kituo cha kupanda na kushuka
na hivyo kuongeza mzunguko wa wateja katika eneo hilo, na kwamba utekelezaji wa
maelekezo hayo umeshaanza kufanyiwa kazi na Sumatra.
Akizungumza na
wafanyabiashara ya usafiri wa mabasi katika Stendi Kuu ya mabasi ya mikoani,
Mkurugenzi Kunambi aliwaambia kuwa, Manispaa kwa kushauriana na uongozi wa Mkoa
na wadau kama Sumatra imepanga kuhamishia Stendi hiyo katika eneo la Chaduru au
kwenye eneo la viwanja vya Nanenane vilivyopo Kata ya Nzuguni barabara kuu ya
Dodoma-Dar es Salaam.
Alisema Manispaa
itazungumza na uongozi wa wasafirishaji ili kupata mapendekezo yao juu ya eneo rafiki zaidi miongoni mwa maeneo
hayo mawili.
Kwa upande wake, Naibu
Waziri Mavunde aliwataka wote walioathiriwa na zoezi hilo la bomoabomoa wawe
watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati Mamlaka na Viongozi wakifanya juhudi
za makusudi kuwatafutia maeneo rafiki kwa shughuli zao huku Naibu Meya Ngede
akiwahakikishia kuwa Baraza la Madiwani litasimamia kikamilifu suala la
upatikaaji wa maeneo hayo.
Thursday, December 7, 2017
MKURUGENZI MANISPAA YA DODOMA AMALIZA HOFU YA WAFANYABIASHARA 2,500
| Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya DodomaJumanne Ngede akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba Mjini Dodoma jana ambapo alifuatana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi. |
Subscribe to:
Posts (Atom)




