Friday, October 27, 2017
Tuesday, October 24, 2017
WAKUU WA IDARA MANISPAA YA DODOMA WAINGIA MTAANI KUSAKA KODI
| Kiongozi wa kikosi kazi cha Wakuu wa Idara Dickson Kimaro (wa pili kushoto ) akimuhoji mmoja wa Wafanyabiashara wa Eneo la 'Mambo Poa' wakati wa zoezi la uhakiki wa nyaraka mbalimbali za biashara. |
| Mmoja wa wafayabiashara ya chakula maarufu Mama Lishe (kulia) akilipa kodi kwa Maafisa wa Manispaa ya Dodoma wakati wa zoezi la kuhakiki nyaraka za kisheria za kuendesha biashara. |
............................................
MENEJIMENTI
ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imeanza zoezi la uhakiki wa nyaraka
mbalimbali kwa wafanyabiashara waliopanga vibanda vya biashara vinavyomilikiwa
na Manispaa hiyo, ambapo wakuu wa Idara wanatekeleza zoezi hilo kwa kupita
katika vibanda vyote vilivyopangishwa kwa wafanyabiashara.
Nyaraka
zinazohakikiwa ni mikataba ya upangishaji wa chumba cha biashara na leseni za
biashara husika, ambapo maeneo mengine kama viwanda vya matofali, maeneo ya
kuoshea magari, na maeneo ya kuchomelea vyuma pia yatahusishwa katika uhakiki
huo ili kujiridhisha endapo biashara hizo zinaendeshwa kwa kuzingatia sheria na
taratibu kama inavyopaswa.
Zoezi
hilo la siku tatu limeanza vizuri ambapo baadhi ya Wafanyabiashara ambao
mikataba yao ya upangishaji ilimalizika wameonesha ushirikiano kwa kulipia huku
wengine wakifungiwa maduka kwa kushindwa kufanya hivo.
Monday, October 23, 2017
Friday, September 29, 2017
MANISPAA YA DODOMA YAANZA KUANDAA HATI MILIKI ZA ARDHI ZA MIAKA 99 KWA KASI, BARAZA LA MADIWANI LAPONGEZA
.........................................................
HALMASHAURI ya Manispaa ya
Dodoma imekamilisha uandaaji wa hati 912 za umiliki wa ardhi za miaka 99 kama
ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli Mei
15 mwaka huu wakati akitoa tamko la kuivunja iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji
Makao Makuu Dodoma (CDA) na shughuli zote kuhamishiwa katika Manispaa ya
Dodoma.
Akizungumza katika kikao
cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichopokea taarifa
rasmi ya makabidhiano ya majukumu ya iliyokuwa CDA kuhamia Manispaa ya Dodoma
jana, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Godwin Kunambi aliwaambia Madiwani na wananchi
kwa ujumla waliohudhuria Baraza hilo kuwa, hatua hiyo imefikiwa katika kipindi
cha miezi miwili ya Julai na Agosti, huku akiahidi kuwa,Manispaa hiyo itaendelea kutoa huduma hiyo
na nyingine kwa kasi inayoendana na matarajio ya wananchi.
Alisema kati ya hati hizo,
hati 674 zilizowasilishwa kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Wizara ya Ardhi zimeshasajiliwa
na zipo tayari kwa ajili ya kukabidhiwa kwa wananchi husika, huku hati 238
zikiwa katika hatua ya kukaguliwa ili zisainiwe.
Alifafaua zaidi kuwa,
uandaaji huo wa hati unaenda sambamba na utoaji wa vibali vya ujenzi kwa
haraka, ambapo mchakato wa kutoa kibali cha ujenzi unakamilishwa ndani ya siku
saba tu baada ya maombi kupokelewa mpaka muombaji anakabidhiwa kibali chake.
Kufuatia taarifa hiyo, wajumbe
wa Baraza la Madiwani wakiongozwa na Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki
Profesa Davis Mwamfupe wameipongeza Menejimenti ya Halmashauri na watumishi
wote na kuwataka waendelee na juhudi hizo ili pamoja na mambo mengine kuufanya
mji wa Dodoma ukue kwa kasi kwa kuwawezesha wananchi na wadau wengine kujenga.
Monday, September 25, 2017
MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA SEMINA YA SIKU MOJA YA WENYEVITI NA WATENDAJI WA MITAA MANISPAA YA DODOMA SEPTEMBA 16, 2017 KATIKA UKUMBI WA ST GASPER MJINI DODOMA
| Baadhi ya Wakuu wa Idara na wajumbe wengine wakifuatilia ufunguzi wa Semina hiyo. |
| Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo. |
| Baadhi ya Wenyeviti na Watendaji wakifuatilia Semina. |
| Afisa kutoka Idara ya Utumishi na Utawala Agatha Kalesu akitoa mada kuhusu majukumu ya Wenyeviti wa Mitaa. |
| Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji Joachim Henjewele akitoa mada. |
| Mchumi wa Manispaa Shaaban Juma akitoa mada. |
| Mganga Mkuu wa Manispaa Thom Mtoi akitoa mada. |
| Mmoja ya wajumbe akichangia mada. |
| Mmoja ya Wajumbe akitoa mchango wake. |
Monday, September 18, 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)



