|
Katibu wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmshauri ya Manispaa ya Dodoma ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Godwin Kunambi (kushoto) akiwasilisha taarifa ya Katibu mbele ya wajumbe wa Baraza hilo katika Mkutano wa kawaida wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2016/2017 jana katika ukumbi wa Manispaa. Kushoto kwake ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Jumanne Ngede |
|
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma katika Ukumbi wa Manispaa hiyo jana.
|
|
Diwani wa Kata ya Mtumba Manispaa ya Dodoma Edward Maboje akichangia taarifa iliyowasilishwa na Katibu wa Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo Godwin Kunambi iliyojumuisha agizo la Rais Dokta John Magufuli kuhusu uongozi wa Mkoa na wadau wote kuchunguza na kuishauri Serikali endapo kuna haja ya kuendelea au kutoendelea kuwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao (CDA). Madiwani kwa ujumla wao wamependekeza Mamlaka hiyo ivunjwe.
|
|
Baadhi ya Wataalam wa Manispaa ya Dodoma wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo katika Ukumbi wa Manispaa jana. PICHA ZOTE: RAMADHANI JUMA
|
Na Ramadhani Juma
OFISI YA MKURUGENZI
MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wameelezea
kufurahishwa kwao na agizo alilotoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dokta John Pombe Magufuli kuhusu kuundwa kwa timu itakayokuwa na
kujumu la kufanya kuchunguza na kuishauri Serikali endapo kuna haja ya kuendelea
kuwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) katika kuendeleza mji wa
Dodoma au jukumu hilo lifanywe na Halmashauri ya Manispaa kama ilivyo katika
Manispaa zote nchini.
Wakichangia taarifa ya Katibu wa Baraza la Madiwani la Manispaa
ya Dodoma Godwin Kunambi ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo jana,
wajumbe wa Baraza hilo walidai kuwa sasa imefikia wakati Mamlaka hiyo uvunjwe
kwani imekuwa ikisababisha migogoro mingi ya ardhi badala ya kuupanga Mji huo
kwani ndio jukumu lao la msingi.
Madiwani wote waliopata fursa ya kuchangia taarifa hiyo
walieleza kuwa, wananchi wa Manispaa ya Dodoma wamechoshwa na uwepo wa Mamlaka
ya CDA na kwamba imewanyanyasa kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuwapora ardhi
zao bila kuzingatia sheria na taratibu.
Hivi karibuni
Mheshimiwa Rais Dokta John Magufuli akiwa Mjini Dodoma aliagiza pamoja na mambo
mengine, kufanywa majadiliano kati ya wadau ambao ni uongozi wa Mkoa, Mamlaka
ya Ustawishaji (CDA), Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Wizara ya Ardhi na mamlaka
zote zinazohusika ili ziiishauri Serikali juu ya umuhimu wa kuendelea au
kutoendelea na Mamlaka ya hiyo.