.....................................................
MKURUGENZI
wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi ameahidi kuwakatia Bima ya
Afya wafanyakazi 133 wanaosafisha mitaa na barabara zote za Mji wa Dodoma ili
wawe na uhakika wa matibabu wao na familia zao.
Alitoa
ahadi hiyo jana alipofanya mkutano na wafanyakazi hao katika viwanja vya
Nyerere katikati ya Mji wa Dodoma ambapo pia aliwapatia fedha taslimu Shilingi
10,000 na mche mmoja wa sabuni kila mmoja kama zawadi kuelekea mwisho wa mwaka
2017.
Mkurugenzi
Kunambi alisema kuwa, yeye kwa niaba ya Uongozi wa Manispaa ametoa zawadi na ahadi ya kuwakatia Bima ya
matibabu baada ya kufurahishwa na uchapa kazi wao unaopelekea mitaa na barabara
za Mji kuwa safi na kupendeza muda wote.
“Hiki
tunachowapa leo hakina thamani yeyote kwa kazi kubwa mnayoifanya, bali ni
kuonesha kuguswa kwetu tu kama Manispaa…ninyi ni kundi maalum na ni wafanyakazi
muhimu sana” alisema Kunambi akizungumza na watumishi hao.
“Nimefurahi
kukutana na kuzungumza na ninyi kipindi hiki cha mwisho wa mwaka…nawaahidi
mapema mwakani Manispaa itawakatika Bima za Afya wote itakayomwawezesha kila
mmoja kutibiwa yeye na wategemezi wake watatu” alifafanua.
Kwa
upande wao, wafanyakazi hao ambao wengi wao ni akina Mama walimshukuru
Mkurugenzi huyo kwa niaba ya Manispaa kwa kuwajali licha ya kuwa wao ni
watumishi wa kada ya chini na wanaofanya kazi kwa mkataba isiyo ya kudumu.
“Tumefurahi
sana leo Mkurugenzi wetu umekuja kuongea na sisi na kutupa zawadi na fedha tena
katika kipindi cha Sikukuu za mwisho wa mwaka...umetujali sana na sisi tunakuombea
kwa Mugu”… alisema mmoja ya akia mama hao akimshukuru Mkurugenzi wa Manispaa.