Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiazungumza kabla ya uzinduzi wa programu ya upadaji miti ili kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani iliyofanyika kwenye chanzo cha maji cha Mzakwe Kata ya Makutupora Mjini Dodoma jana. PICHA ZOTE: RAMADHAI JUMA-OFISI YA MKURUGENZI MANISPAA YA DODOMA
......................................................................
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezitaka Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kutunga
Sheria Ndogo zitakazomtaka kila Mkazi wa eneo katika Mkoa huo kupanda miti ili
kupambana na mabadiliko ya hali tabia Nchi.
Makamu wa Rais ametoa agizo hilo
kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani iliyofanyika
Desemba 21 mwaka huu katika eneo la Mzakwe Kata ya Makutupora Manispaa ya
Dodoma.
Alisema upandaji miti si kwa ajili ya
kuhifadhi mazingira tu bali ni fursa ya kiuchumi, kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi ambapo alitolea mfano mti mmoja uliokomaa unaweza kunyonya kiasi
cha kilogramu 150 za gesi ya hewa ya ukaa kwa mwaka na hivyo kusaidia kupunguza
joto kwenye uso wa dunia, na pia kusaidia kuboresha afya ya mwili na akili.
“Ni dhahiri, kampeni hii ya kuifanya
mji wa Dodoma kuwa wa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu, Dkt. John
Pombe Magufuli wa kuhamishia Makamo Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja
Dodoma kwa vitendo.” Alisema.
Akihojiwa na Vyombo vya Habari wakati
wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi
alisema Manispaa ya Dodoma imejipanga kuugeuza Mji wa Dodoma kuwa kivutio
kikubwa kimazingira kwani pamoja na kuhakikisha inasimamia na kutekeleza kwa
ukamilifu program iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, pia Manispaa itatenga eneo
maalum la ukanda wa kijani (Green Belt) ili kuufanya Mji huo kuwa wa kipekee
nchini.
|
No comments:
Post a Comment