Zoezi la usafi likiendelea katika Mtaa za Zahanati Kata ya Kikuyu Kaskazini Manispaa ya Dodoma. |
...............................................
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dokta
Binilith Mahenge ameahidi kutoa motisha ya Shilingi 1,000,000 kwa wakazi wa
mtaa wa Zahati uliopo Kata ya Kikuyu Kaskazini katika Manispaa ya Dodoma
kufuatia wakazi hao kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi wa Mazingira unaofanyika
kila Jumamosi katika Manispaa hiyo.
Mheshimiwa Mahenge alitoa
ahadi hiyo wakati alipowaongoza wakazi hao katika zoezi la usafi wa Mazingira
katika Mtaa huo mwishoni mwa wiki, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kufanya usafi
wa Mazingira kila Jumamosi aliyoianzisha yeye mara tu baada ya kuhamishiwa Mkoa
humo, kwa lengo la kuuweka Mji Mkuu wa Nchi katika hali ya usafi wakati wote.
Alisema fedha atakazowapa
wakazi wa Mtaa huo ni motisha na kuwaunga mkono kwa juhudi walizoonesha na
kwamba zitawasaidia katika kuboresha hali ya usafi katika eneo lao kwa kununua
vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi.
Alisema amefurahishwa na
namna wakazi wa Mtaa wa Zahati walivyojitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo
na kutoa wito kwa wakazi wa maeneo mengine katika Manispaa kuiga mfano huo ili
kwa pamoja waweze kuufanya Mji wa Dodoma kuwa namba moja kwa usafi wa Mazingira
nchini.
No comments:
Post a Comment