Thursday, June 22, 2017
Thursday, June 8, 2017
'KITIMOTO' MARUFUKU MAKAO MAKUU DODOMA
Katika kipindi cha zuio:
- Hakuna mnyama yeyote jamii ya nguruwe (Ngiri, nguruwe pori au nguruwe wa kufugwa) ataruhusiwa kuingia, au kutoka nje ya eneo la Wilaya ya Dodoma pasipokuwa na ruhusa ya maaandishi kutoka kwa Daktari wa Mifugo wa Wilaya ya Dodoma.
- Pia hakuna bidhaa inayotokana na nguruwe, ikiwemo mbolea, kinyesi, mkojo na damu kitakacho ruhusiwa kuingia au kutoka nje ya Wilaya ya Dodoma pasipokuwa na ruhusa ya maandishi kutoka kwa Daktari wa Mifugo wa Wilaya ya Dodoma Mjini.
- Aidha, hakuna mnyama yeyote wa jamii iliyotajwa hapo juu atakayekusanywa kwa ajili ya biashara pasipokuwa na ruhusa ya maandishi kutoka kwa Daktari wa Mifugo wa Wilaya ya Dodoma.
- Uchinjaji wa nguruwe ndani ya Wilaya ya Dodoma, utafanyika chini ya usimamizi madhubuti wa mtaalam wa afya za mifugo mwenye dhamana.
MKUU WA WILAYA YA DODOMA CHRISTINE MNDEME KUVILEA VIKUNDI VYA USAFISHAJI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MANISPAA YA DODOMA
MKUU wa wilaya ya Dodoma Mheshimiwa Christine Mndeme akikagua mabanda ya wadau wa utunzaji wa Mazingira kwa njia ya ufugaji nyuki. |
MKUU wa wilaya ya Dodoma Mheshimiwa Christine Mndeme akikagua mabanda ya wadau wa utunzaji wa Mazingira kwa njia ya kuchoma mkaa bila kukata miti badala yake wanatumia pumba. |
MKUU wa wilaya ya Dodoma Mheshimiwa Christine Mndeme akikabidhi vifaa vya usafishaji wa mazingira kwa viongozi wa vikundi vya usafishaji wa Mazingira Manispaa ya Dodoma |
MKUU wa wilaya ya Dodoma Mheshimiwa Christine Mndeme amekubali jukumu la kuwa mlezi wa vikundi mbalimbali vya usafi na utunzaji wa Mazingira vilivyopo katika Manispaa ya Dodoma, hatua ambayo pia itamuweka karibu zaidi na vikundi hivyo katika kazi muhimu ya kuuweka mji huo katika hali ya usafi na kuvutia ikizingatiwa kuwa ndio Makao Makuu ya Nchi na tayari Serikali imeshahamia mjini humo.
Mheshimiwa Mndeme alitangaza hatua hiyo wakati wa
maadhimisho ya kilele cha Siku ya Mazingira Duniani Juni 5 mwaka huu kwa ngazi
ya Wilaya yaliyofanyika katika viunga vya Bustani ya Nyerere Square mjini
Dodoma.
Katika sherehe hizo,
Mkuu huyo wa Wilaya pia alikagua mabanda ya wadau wa utunzaji wa Mazingira
na kugawa vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kwa vikundi nane vya usafi vyenye thamani ya shilingi milioni 4.
Sherehe hizo
zilihudhuriwa pia na Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede, Ofisa
Mazingira wa Manispaa hiyo Dickson Kimari amabaye alimuwakilisha pia Mkurugenzi
wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi, Ofisa Mazingira kutoka Idara ya Mazingira
katika Ofisi ya Makamu wa Rais Timotheo Mande pamoja na wadau wengine.
Monday, June 5, 2017
OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAPONGEZA JUHUDI ZA KUTUNZA MAZINGIRA MANISPAA YA DODOMA
OFISI ya Makamu wa Rais imepongeza
jitihada zinazofanywa na Manispaa ya Dodoma katika kuuweka mji wa Dodoma katika
hali ya usafi ikiwemo kuimarisha vikundi vya usafi kwa kuwapatia vifaa
mbalimbali vya kufanyia usafi.
Pongezi hizo zilitolewa jana na Ofisa
Mazingira wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Timotheo Mande
alipokuwa akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani
yaliyofanyika kwa ngazi ya Wilaya katika viwanja vya ‘Nyerere Square’ Manispaa
ya Dodoma.
Alielezea kufurahishwa na
namna Manispaa inavyoshirikiana na kuvisaidia vikundi vya usafi na utunzaji wa
Mazingira ambapo katika maadhimisho
hayo alishuhudia vikundi nane vikikabidhiwa vifaa mbalimbali vya usafi vyenye
thamani ya shilingi milioni 4.
WAFANYABIASHARA BUSTANI YA UHURU KUONDOLEWA
Bustani ya 'Independence Square' katika Manispaa ya Dodoma inavyoonekana kwa sasa ikiwa imezungukwa na wafanyabiashara ndogo. |
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christine Mndeme akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya hafla ya Ufunguzi |
Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa hafla hiyo |
MKUU wa Wilaya ya
Dodoma Christine Mndeme amesema wafanyabiashara ndogo waliozunguka eneo la
bustani ya Uhuru katika Manispaa ya Dodoma wataondolewa na kuhamishiwa katika
masoko ya Sabasaba na Bonanza ili eneo hilo libaki wazi kwa ajili ya kuupezesha
mji wa Dodoma na kuufanya uvutie zaidi ili kufikia lengo la kuboreshwa kwa
bustani hizo.
Alitoa ahadi hiyo
alipokuwa akifungua rasmi bustani hiyo leo Juni 5, 2017 ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya kilele cha Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika katika
viwanja vya ‘Nyerere Square’ Manispaa ya Dodoma.
Bustani hiyo inahudumiwa
na Benki ya Biashara ya Akiba (ACB) kwa makubaliano maalum na Manispaa ya
Dodoma, ambapo meneja wa tawi la Benki hiyo John Magigita imeeleza kuwa
changomoto kubwa ni kuwabustani hiyo imezungukwa na wafanyabiashara ndogo hali
inayopelekea kupoteza mvuto wake na kutoonekana vizuri.
Naibu Meya wa
Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede amesema Manispaa ya Dodoma itashirikiana na
Ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya katika kuwahamisha wafanyabiashara hao na
kutafutia nafasi katika masoko mengine baada ya soko la majengo kujaa hali
iliyopelekea wao kupanga bidhaa zao katika viunga vya bustani hiyo.
Naye Ofisa Mazingira na Usafishaji
wa Manispaa ya Dodoma ambaye
alimuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Godwin Kunambi katika Hafla hiyo
fupi ya ufunguzi, alisema kuwa Manispaa imejipanga kuhakikisha mji wa Dodoma
unakuwa katika hali ya usafi muda wote kwani tayari Dampo jipya la kisasa la
kuzika taka lililopo katika eneo ya Chidaya limeshaanza kazi na kwamba
watendaji wa Kata watashirikishwa kikamilifu katika kusimamia sheria za usafi
na mazingira katika maeneo yao.
Subscribe to:
Posts (Atom)