MKUU wa wilaya ya Dodoma Mheshimiwa Christine Mndeme akikagua mabanda ya wadau wa utunzaji wa Mazingira kwa njia ya ufugaji nyuki. |
MKUU wa wilaya ya Dodoma Mheshimiwa Christine Mndeme akikagua mabanda ya wadau wa utunzaji wa Mazingira kwa njia ya kuchoma mkaa bila kukata miti badala yake wanatumia pumba. |
MKUU wa wilaya ya Dodoma Mheshimiwa Christine Mndeme akikabidhi vifaa vya usafishaji wa mazingira kwa viongozi wa vikundi vya usafishaji wa Mazingira Manispaa ya Dodoma |
MKUU wa wilaya ya Dodoma Mheshimiwa Christine Mndeme amekubali jukumu la kuwa mlezi wa vikundi mbalimbali vya usafi na utunzaji wa Mazingira vilivyopo katika Manispaa ya Dodoma, hatua ambayo pia itamuweka karibu zaidi na vikundi hivyo katika kazi muhimu ya kuuweka mji huo katika hali ya usafi na kuvutia ikizingatiwa kuwa ndio Makao Makuu ya Nchi na tayari Serikali imeshahamia mjini humo.
Mheshimiwa Mndeme alitangaza hatua hiyo wakati wa
maadhimisho ya kilele cha Siku ya Mazingira Duniani Juni 5 mwaka huu kwa ngazi
ya Wilaya yaliyofanyika katika viunga vya Bustani ya Nyerere Square mjini
Dodoma.
Katika sherehe hizo,
Mkuu huyo wa Wilaya pia alikagua mabanda ya wadau wa utunzaji wa Mazingira
na kugawa vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kwa vikundi nane vya usafi vyenye thamani ya shilingi milioni 4.
Sherehe hizo
zilihudhuriwa pia na Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede, Ofisa
Mazingira wa Manispaa hiyo Dickson Kimari amabaye alimuwakilisha pia Mkurugenzi
wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi, Ofisa Mazingira kutoka Idara ya Mazingira
katika Ofisi ya Makamu wa Rais Timotheo Mande pamoja na wadau wengine.
No comments:
Post a Comment