Thursday, December 7, 2017

MKURUGENZI MANISPAA YA DODOMA AMALIZA HOFU YA WAFANYABIASHARA 2,500

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba (hawapo pichani) Mjini Dodoma jana ambapo aliwahakikishia kuwa hawatahamishwa katika soko hilo. 

Sehemu ya Wafanyabiashara ya Manispaa ya Dodoma wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa Mkurugenzi huyo na wafayabiashara wa soko hilo jana.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya DodomaJumanne Ngede akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba Mjini Dodoma jana ambapo alifuatana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi. 

3 comments:

  1. Kati ya mambo ambayo tunapaswa kujivunia katika uongozi wa awamu ya tano ni utawala wenye kauli zinazotekelezeka. Manispaa sasa imekuwa moja kati ya mahali salama ambako wananchi wanaweza kukimbilia na kupata ahueni. Hongera sana MD Kunambi na tuimu yako kwa kazi nzuri mnazozifanya. Manispaa sasa ina haki ya kuwa Jiji.

    ReplyDelete
  2. Miongoni mwa mambo ambayo wana Dodoma tunapaswa kujivunia kutoka kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ni pamoja na uhakika wa Ardhi na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa migogoro ya ardhi katika kata zote 41 za Manispaa ya Dodoma.

    Uhakika wa huduma za Afya na Maji kwa wakazi wa Manispaa ya Dodoma, maboresho makubwa katika sekta ya Elimu hususan miundombinu, upatikanaji wa walimu, mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia na ushiriki wa wananchi katika mikutano ya kimaamuzi katika ngazi mbalimbali.

    Hali hii imeifanya sasa Manispaa kufanya kazi kwa kujiamini zaidi kutokana na kuungwa mkono na wananchi badala ya kufanya kazi kwa kujiandaa kujibu hoja za wananchi. Ni dhahiri kwamba kila maendeleo yanakumbana au kuandamana na changamoto. (Baadhi au wachache huumia ili wengi wanufaike) hali hiyo haiwezi kukwepeka popote duniani. Tuendelee kuunga mkono na zaidi kuielimisha jamii kabla ya kutoa maamuzi ili jamii iwe sehemu kubwa ya maamuzi na watendaji kusimamia utekelezaji. Manispaa ya Dodoma inastahili pongezi katika haya! Tuungane sote katika kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 9 Desemba 2017.

    ReplyDelete
  3. Kwa niaba ya Manispaa napokea pongezi zako na naamini zitatuzishia nguvu ya kuendelea kuhudumia wananchi wetu kwa uwezo wetu wote!Asante!

    ReplyDelete