Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Uhuru Manispaa ya Dodoma Ally Kheri (kulia) akishiriki zoezi la usafi wa Mazingira katika Mtaa wa Barabara ya 8 katikati ya Mji wa Dodoma wakati wa zoezi la usafi wa Mazingira unaofanywa kila Jumamosi ikiwa ni Kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Daktari Binilith Mahenge. |
........................................
HALMASHAURI ya Manispaa ya
Dodoma imepanga kutumia askari wa Mgambo 30 watakaokuwa wanafanya doria katika viunga
vya Mji ili kudhibiti watu wanaochafua mazingira kwa kutupa taka ovyo ikiwa ni
namna mojawapo ya kuhakikisha mji huo unakuwa safi wakati wote ikizingatiwa kuwa ndiyo Makao Makuu ya Nchi.
Hatua hiyo inafuatia
kampeni ya usafi wa mazingira iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Daktari
Binilith Mahenge ya kufanya usafi siku ya Jumamosi kila wiki.
Akizungumza wakati wa zoezi
la usafi mwishoni mwa Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin
Kunambi amesema askari Mgambo 30 waliofuzu mafunzo wako tayari na kwamba
Manispaa inatarajia kuanza kuwatumia wiki hii ya kwanza ya mwezi Desemba.
Aliwashauri wakazi wa
Dodoma na wageni kujiepusha na utupaji wa taka ovyo, na kwamba atakayebainika
na kuthibitika kufanya hivyo atatozwa faini kati ya Shilingi 50,000 hadi 300,000
kulingana na mazingira ya tukio papo hapo na endapo atashindwa kulipa
atatumikia kifungo cha miezi sita gerezani.
No comments:
Post a Comment