BARAZA la Madiwani wa Manispaa ya Dodoma limempongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta John Magufuli kwa hatua yake ya kuivunja rasmi iliyokuwa Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Dodoma (CDA) na kwamba
hatua ni maamuzi muhimu na sahihi kwa maendeleo ya Manispaa na Mkoa wa Dodoma kwa ujumla.
Wajumbe wa Baraza hilo likiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye
ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Jumanne
Ngede walikutana jana kwenye ukumbi wa Manispaa kwa ajili ya Mkutano Maalum wa kuzungumza na vyombo vya
Habari na kutoa tamko rasmi la
kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua hiyo.
Walidai hatua hiyo itafungua milango kwa wawekezaji wengi kuwekea
Dodoma kutokana na taratibu za kupataji
na umiliki wa ardhi kuboreshwa chini ya Manispaa, ikiwemo utolewaji wa hati za
umiliki wa ardhi za miaka 99 badala zile za miaka 33 zilizokuwa zikitolewa na
iliyokuwa CDA.
Mei 15 mwaka huu, Mheshimiwa Rais Dokta John Magufuli alisaini
tamko la Amri ya Rais la kuivunja iliyokuwa CDA baada ya kujiridhisha kuwa kwa
sasa hakuna mahitaji ya kuwa na mamlaka hiyo iliyoanzishwa kwa Amri ya Rais mwaka
1973, na kwamba shughuli, mali, na watumishi 284 wanakuwa chini ya Manispaa ya
Dodoma.
No comments:
Post a Comment