Meneja wa Dampo la Kisasa linalotumia teknolojia ya kuzika taka ngumu (Landa Fill) katika Manispaa ya Dodoma John Chiwanga ( kushoto ) akitoa maelezo kwa Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mstahiki Maabad Hoja (wa pili kulia) na baadhi ya Madiwani na Wataalam wa Manispaa hiyo walipokuwa katika ziara ya Mafunzo jana Aprili 27, 2017. Wa kwanza kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede.
|
MKURUGENZI wa Manispaa
ya Dodoma Godwin Kunambi ametoa wito kwa Halmshauri nchini kuwekeza katika
Manispaa ya Dodoma kama njia mojawapo ya kujiongezea mapato ya ndani.
Ametoa wito huo jana wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara
ya mafunzo ya Madiwani na Wataalam wa Manispaa ya Kigamboni Mkoa wa Dar es
Salaam waliyoifanya katika Manispaa ya Dodoma.
Kunambi aliwaeleza wageni
hao kuwa, Manispaa ya Dodoma ina fursa nyingi za uwekezaji ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa hoteli za kisasa, majengo ya Ofisi, na miundombinu mingine
ikizingatiwa kuwa kuna rasilimali ardhi ya kutosha na sasa ni Makao Makuu ya
Nchi.
Msafara wa watu 20 wakiwemo Madiwani na Wataalam kutoka
Manispaa ya Kigamboni ukiongozwa na Meya
wa Manispaa hiyo Mstahiki Maabad Hoja walifanya ziara ya mafunzo juu ya usafi wa
Mazingira na uhifadhi wa taka kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kuzika taka
ardhini (Land Filling) ambapo Manispaa ya Dodoma inafanya vizuri kupitia Dampo
lililopo katika Kata ya Ntyuka katika Manispaa hiyo.
Pia ziara yao ililenga kulijifunza kuhusu suala la utozaji na
ukusanyaji wa kodi mbalimbali unaofanywa na Manispaa.
No comments:
Post a Comment