Kiongozi wa kikosi kazi cha Wakuu wa Idara Dickson Kimaro (wa pili kushoto ) akimuhoji mmoja wa Wafanyabiashara wa Eneo la 'Mambo Poa' wakati wa zoezi la uhakiki wa nyaraka mbalimbali za biashara. |
Mmoja wa wafayabiashara ya chakula maarufu Mama Lishe (kulia) akilipa kodi kwa Maafisa wa Manispaa ya Dodoma wakati wa zoezi la kuhakiki nyaraka za kisheria za kuendesha biashara. |
............................................
MENEJIMENTI
ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imeanza zoezi la uhakiki wa nyaraka
mbalimbali kwa wafanyabiashara waliopanga vibanda vya biashara vinavyomilikiwa
na Manispaa hiyo, ambapo wakuu wa Idara wanatekeleza zoezi hilo kwa kupita
katika vibanda vyote vilivyopangishwa kwa wafanyabiashara.
Nyaraka
zinazohakikiwa ni mikataba ya upangishaji wa chumba cha biashara na leseni za
biashara husika, ambapo maeneo mengine kama viwanda vya matofali, maeneo ya
kuoshea magari, na maeneo ya kuchomelea vyuma pia yatahusishwa katika uhakiki
huo ili kujiridhisha endapo biashara hizo zinaendeshwa kwa kuzingatia sheria na
taratibu kama inavyopaswa.
Zoezi
hilo la siku tatu limeanza vizuri ambapo baadhi ya Wafanyabiashara ambao
mikataba yao ya upangishaji ilimalizika wameonesha ushirikiano kwa kulipia huku
wengine wakifungiwa maduka kwa kushindwa kufanya hivo.
No comments:
Post a Comment