WAKAZI wa Manispaa ya
Dodoma wameshauriwa kuhudhuria mikutano ya Baraza la Madiwani ili kupata taarifa
za miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Manispaa yao na kujua kazi
inayofanywa na Madiwani waliowachagua.
Wito huo umetolewa na Naibu
Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede kuelekea Mkutano wa Baraza hilo wa
kisheria kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 utakaopokea taarifa mbalimbali za Manispaa
hiyo kitakachonyika Oktoba 31 mwaka huu katika ukumbi wa Manispaa.
Naibu Meya Ngede alitoa
wito huo wakati alipoongoza Mkutano wa awali wa Baraza la Madiwani la Manispaa
hiyo lililopokea taarifa za utekelezaji wa miradi kutoka katika Kata zote 41 za
Manispaa ya Dodoma Oktoba 25 mwaka huu.
Aliiagiza Ofisi ya
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuongeza matangazo kwa wananchi kuhusu tarehe ya Mkutano huo
ili waweze kuhudhuria kutokana na umuhimu wa mkutano huo ambao ni wa
wazi.
No comments:
Post a Comment