Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia mkutano wa Baraza jana katika ukumbi wa Manispaa. |
Baadhi ya Wageni Waalikwa wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Robert Mwinje, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma White Zuberi (wa pili kushoto), na Mwneyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Danford Chisomi (wa pili kulia). Kushoto ni Meya wa Jiji la Mbeya Mstahiki David Mwasilindi.
|
..................................................
HALMASHAURI zote nane za
Mkoa wa Dodoma zimekubaliana kuwa na utaratibu wa ziara za kubadilishana uzoefu
hususan katika uendeshaji wa vikao na mikutano ikiwemo Baraza la Madiwani.
Hayo yalisemwa jana na Meya
wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe wakati
akiwatambulisha baadhi ya Wenyeviti na Wataalam wa Halmashauri za Wilaya za
Mkoani humo waliohudhuria mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Dodoma
ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa ushirikiano huo.
Mkutano huo uliofanyika
katika ukumbi wa Manispaa ya Dodoma, ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kongwa Mheshimiwa White Zuberi Mwanzalila ambaye pia ndiye
Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mheshimiwa
Danford Chisomi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mheshimiwa Samweli
Kaweya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bahi Rachel Chuwa.
Halmashauri zinazounda Mkoa
wa Dodoma ni Manispaa ya Dodoma, Bahi, Chamwino, Kongwa, Mpwapwa, Kondoa Mji,
Kondoa Vijijini, na Chemba.
No comments:
Post a Comment