Diwani wa Kata ya Msalato Ally Mohamed akitoa neno wakati wa sherehe hizo |
Kaimu wa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Dodoma Rukia Nyange akitoa neno. |
..................................................
HALMASHAURI ya Manispaa ya
Dodoma imezindua Mpango Mkakati wa kuwawezesha kiuchumi Wanawake na akina Mama
wa Manispaa hiyo ili wajikwamue katika changamoto mbalimbali za maisha yao ya
kila siku.
Mpango Mkakati huo unaotarajiwa
kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2018, ulizinduliwa
jana Machi 8, 2018 ambapo sherehe za uzinduzi zilienda sambamba na maadhimisho
ya kilele cha siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika katika Kata ya Msalato
Mjini Dodoma.
Akizindua Mpango Mkakati
huo, Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Dodoma Fatma Tawfiq alitoa wito kwa
Wanawake kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuwa kimoja ili kupambana na
changamoto zinazowakabili ikiwemo za kiuchumi.
Aliwataka pia kuwa tayari
kugombea na nafasi mbalimbali za uongozi ili wawe katika nafasi za maamuzi, na
kwamba waanze na uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Mwakani
kabla ya ule Mkuu wa mwaka 2020.
Kwa upande wake, Mratibu wa
Dawati la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wa Manispaa ya Dodoma Hidaya Mizega ambaye
alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Godwin Kunambi katika sherehe hizo alisemakuwa,
Mpango Mkakati huo ndio dira ya kuwainua wanawake wa Manispaa ya Dodoma
kiuchumi na kwamba yataandaliwa majukwaa mbalimbali ya Wanawake ili
kuutambulisha kwa wadau.
“Wanawake wataongozwa jinsi
ya kuunda vikundi vingi vya kuichumi ili kupata fursa mbalimbali wakiwa pamoja…kwa
sasa Dawati la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi limeanzishwa katika kila Kata ya
Manispaa ya Dodoma” alisema Mizega.
Alisema kuwa miongoni mwa
malengo mahsusi ni kuwa na SACCOS ya akina mama wote wa Wilaya ya Dodoma, hivyo
baada ya kipindi cha miaka mitatu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati huo
kumalizika, itafanywa tathmini ya kina kuhusu mafanikio na changamoto
zilizojitokeza ili zifanyiwe kazi.
No comments:
Post a Comment