Sehemu ya Baa Tango iliyopo eneo la Uhindini katikati ya Mji wa Dodoma nayo ilikumbwa na Bomoa Bomoa iliyoendeshwa na Manispaa ya Dodoma baada ya mmiliki wake kukiuka taratibu za ujenzi. |
Sehemu ya Baa Tango iliyopo eneo la Uhindini katikati ya Mji wa Dodoma nayo ilikumbwa na Bomoa Bomoa iliyoendeshwa na Manispaa ya Dodoma baada ya mmiliki wake kukiuka taratibu za ujenzi. |
Ubomoaji wa vibanda vilivyojengwa kando ya Barabara kuu ya Dodoma-Dar es Salaam ukiendelea wakati wa zoezi lililoendeshwa na Manispaa ya Dodoma jana. |
Afisa Mdhibiti wa Ujenzi wa Manispaa ya Dodoma Ally Bellah akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari juu ya zoezi la bomoa bomoa lililoendeshwa na Manispaa ya Dodoma jana. |
.....................................
BAADHI ya Wakazi wa
Manispaa ya Dodoma wameunga mkono zoezi la kubomoa nyumba na vibanda vilivyojengwa
katika maeneo ya yasiyo rasmi ikiwemo hifadhi za barabara, maeneo ya wazi, na wale
waliojenga katika viwanja wasivyovimiliki linalofanywa na Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma.
Baadhi ya wananchi waliotoa
maoni yao katika maeneo ya Kisasa, Majengo, Nkuhungu, na Kikuyu ambapo zoezi
hilo lilitekelezwa hapo jana, wamesema kumekuwapo na mazoea ya watu kuvamia
maeneo yasiyo rasmi na kuanzisha makazi au vibanda vya biashara japo
linaloharibu taswira ya Mji.
Akizungumza wakati wa zoezi
hilo la siku mbili lililoanza jana, Afisa Mdhibiti Ujenzi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Dodoma Ally Bellah alisema zoezi hilo linafanyika kwa mujibu wa sheria na
kwamba taratibu zote zimefuatwa kabla ya kufikia hatua ya uvunjaji.
“Maeneo yote haya
tunayovunja wahusika walishapewa notisi kwa mujibu wa Sheria lakini wengi wao
wamekaidi…kwa wale waliostahili kupewa fidia walishapewa fidia zao muda mrefu”
alisema.
Bellah ametoa wito kwa
Wakazi wote wa Manispaa ya hata wageni wanaohamia kuepuka kununua ardhi
kienyeji kwani wanaweza kutapeliwa na kuuziwa maeneo ya wazi au yasiyo ya
makazi na kujikuta wakipata usumbufu usio wa lazima.
“Hata wageni wanaohamia
Manispaa ya Dodoma niseme kwamba tunawapenda sana na tunawakaribisha ila watakapohitaji
ardhi au viwanja kwa ajili ya kujenga wahakikishe wanawasiliana na Halmashauri
ya Manispaa ya Dodoma ili wawe salama” alisistiza
Alisema Mji wa Dodoma ni Makao
Makuu ya Nchi hivyo lazima uwe na muonekano wa kuvutia na kwamba zoezi la bomoa
bomoa ni endelevu ili kudhibiti ujenzi holela na kusimamia ujenzi bora kwa
mujibu wa vibali vinavyotolewa.
No comments:
Post a Comment