Baadhi ya Wafanyabiashara Ndogo wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi |
.....................................
Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amekabidhi vitambulisho kwa
Wafanyabiashara ndogo maarufu kama m Machinga wanaofanya shughuli zao katika
soko la jioni ili waweze kufahamiana wakati wa biashara zao na hata kusaidia kuimarisha
masuala ya ulinzi na usalama.
Wafanyabiashara ndogo
wapatao 140 wanaofanya shughuli zao katika eneo la Viwanja vya Nyerere wamekabidhiwa
vitambulisho hivyo na Mkurugenzi huyo katika hafla fupi iliyofanywa katika
viwanja hivyo mchana wa leo.
Akizungumza katika hafla
hiyo, Mkurugenzi Kunambi amewaasa wafanyabiashara hao kuwa na utamaduni wa
kutunza akiba ili kukuza mitaji yao huku akiwaahidi kuwaboreshea mazingira ya
kazi zao na kwamba hakuna kiongozi atakayewaondoa katika maeneo hayo mpaka
watakapatiwa maeneo mbadala na rafiki kwa biashara zao.
“Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli ni rafiki wa Machinga na ameshatoa
maelekezo na nyinyi ni mashahidi…nawaahidi kusimamia maagizo ya Rais ya
kuhakikisha wananchi wanyonge hawanyanyasiki ndani ya Nchi yao” alisema
Kunambi.
Aliwataka wafanyabiashara
kujiandaa kutumia fursa za ujenzi wa stendi mpya na ya kisasa na soko kubwa kwa
ajili ya wafanyabiashara vitakavyojengwa katika Kata ya Nzuguni ili waweze
kukua kibiashara.
“Tunaanza ujenzi wa stendi
kubwa ya kisasa nay a mfano Afrika Mashariki na Kati katika eneo la Nzuguni
Mwezi Machi 2018…ujenzi utakamilika baada ya miezi 24 na utaenda sambamba na
ujenzi wa soko kubwa la kisasa kwahiyo jiandaeni kutumia hizo fursa”
alisisitiza.
No comments:
Post a Comment