Kazi ya ukarabati ikiwa imeanza katika Shule ya Sekondari ya Dodoma |
Kazi ya ukarabati ikiwa imeanza katika Shule ya Sekondari ya Dodoma |
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Graceana Shirima (kushoto) akikagua maeneo mbalimbali yanayofanyiwa ukarabati katika Shule ya Sekondari ya Bihawana iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma jana mara baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa kazi hiyo. TEA imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuikarabati Shule hiyo.
..............................................
SERIKALI kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetoa
zaidi ya shilingi Bilioni 2.1 kwa ajili ya kukarabati Shule za Sekondari za
Bihawana na Dodoma zilizopo Manispaa ya Dodoma ikiwa ni sehemu ya utekezaji wa
mpango wa Serikali wa kuzifanyia ukarabati mkubwa Shule kongwe Nchini.
Kati ya Fedha hizo, zaidi ya Shilingi Bilioni 1.2
zitatumika kukarabati Shule ya Sekondari ya Bihawana pekee na zaidi ya Shilingi
Milioni 900 zitatumika katika Shule ya Sekondari ya Dodoma.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi rasmi wa kazi ya ukarabati katika shule hizo jana, Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa TEA Graceana Shirima alisema kuwa, shughuli ya ukarabati ilitanguliwa
na upembuzi yakinifu wa hali halisi ya mahitaji ya ukarabati uliofanywa na mtaalamu
mshauri ambaye ni Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).
“Baada
ya upembuzi yakinifu, maeneo ya kipaumbele katika ukarabati kwa awamu hii
itahusisha Madarasa, maabara, bwalo na jiko,
vyoo, na mifumo ya umeme, mifumo ya TEHAMA na mifumo na maji safi na
maji taka” alisema Shirima.
Alisema
awamu hii ya ukarabati inatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi minne, na awamu nyingine za ukarabati
zitatekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Dodoma Godwin Kunambi aliishukuru Mamlaka ya Elimu kwa kuzipatia Shule za
Manispaa hiyo Fedha nyingi kwa ajili ya ukarabati huku akitolea mfano wa Shule
ya Wasichana ya Msalato ambayo ilishafanyiwa ukarabati mkubwa mwaka uliopita.
Kunambi aliahidi kuwa, Manispaa ya Dodoma ambaye ndiye mmiliki wa Shule hizo itasimamia
kwa karibu kila hatua ya kazi hiyo.
Baadhi
ya Wanafunzi wa Shule zinazofanyiwa ukarabati wamepongeza hatua ya Serikali ya
kutekeleza mpango huo na kwamba itawaboresha mazingira ya kujifunzia ikiwa ni
pamoja na uimarishaji wa miundombinu muhimu kama umeme, maji, na mabweni.
Mamlaka
ya Elimu Tanzania (TEA), kwa kushirikiana na Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia inatekeleza
Mpango kabambe wa ukarabati wa Shule kongwe 89 za Sekondari Nchini ambao
unafanyika kwa awamu.
No comments:
Post a Comment