.....................................................
HALMASHAURI
ya Jiji la Dodoma inatarajia kutoa takribani shilingi milioni 500 kwa ajili ya
kukopesha vikundi vya Wajasiriamali Wanawake na Vijana kwa mwaka wa fedha
unaomalizika Mwezi Juni, 2018.
Jumla
ya vikundi 137 vinatarajiwa kunufaika na fedha hizo zinazotokana na makusanyo
ya kodi za ndani ya Halmashauri (Own Source) ambapo vikundi vya Wanawake ni 102 na vya vijana 37.
Akizungumza
wakati akitoa semina elekezi kwa viongozi wa vikundi hivyo katika ukumbi wa
Shule ya Sekondari ya Dodoma leo Juni 21, 2018, Kaimu Mkuu wa Idara ya
Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Dodoma Mufungo Manyama aliwaeleza wajumbe kuwa awamu
ya mwisho ya mikopo kwa mwaka huu wa fedha itatolewa katikati ya wiki ijayo
ambapo jumla ya Shilingi milioni 344 zitakabidhiwa kwa vikundi hivyo.
Aliwataka
Wanavikundi hao kuwa makini na matumizi ya fedha wanazokopeshwa na kufanya
marejesho kwa wakati ili wapate fursa ya kukopeshwa zaidi.
Kwa
upande wao, baadhi ya viongozi wa vikundi hivyo waliishukuru Halmshauri ya Jiji
na kuahidi kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili waweze kurejesha kwa
wakati hali itakayopelekea kunufaisha vikundi vingi zaidi.
No comments:
Post a Comment