Wadau mbalimbali katika Maandamano kuelekea Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani leo Juni 5, 2018. |
Mgeni Rasmi Naibu Meya Jumanne Ngede (wa pili kulia) akikagua mabanda ya wadau wa Mazingira |
|
....................................................................
NAIBU
Meya wa Halmshauri ya Jiji la Dodoma Jumanne Ngede ametoa wito kwa kila mkazi
wa Jiji hilo kuhakikisha anatunza Mazingira kwa kupanda miti katika maeneo
yanayomzunguka ili kuunga mkono juhudu za Serikali na wadau kuhakikisha Jiji
linakuwa la kijani kwa manufaa ya viumbe vyote.
Alitoa
wito huo mapema leo asubuhi alipotembelea na kukagua mabanda ya wadau
mbalimbali wa Mazingira walioshiriki kilele cha Maadhimisho ya Siku ya
Mazingira Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere
vilivyopo katikati ya Jiji la Dodoma leo Juni 5, 2018.
Mhe.
Ngede aliwapongeza wadu mbalimbali hususan wanaojihusisha na nishati mbadala
kama Gesi na Sola ambazo matumizi yake yanasaidia kupunguza ukataji wa miti na uharibufu wa misitu kwa
ajili ya kuchoma mkaa unaotumika kwa kazi za jikoni.
Kwa
upande wake, Afisa Mazingira kutoka Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Takangumu
Jiji la Dodoma Ally Mfinanga alisema Halmashauri imekuwa ikishikiana na wadau
mbalimbali ili kuhakikisha kila kundi katika jamii linawajibika katika kutunza
Mazingira.
“Kuna
wadau ambao tunashirikiana nao katika kutunza Mazingira kwa maana ya kupanda
miti na kutunza misitu lakini pia, kama Halmashauri tunajukumu la kusafisha
Mazingira kwa kuondosha taka zinazozalishwa Mjini…haya yote tunayatekeleza kwa
kuwashirikisha pia wadau kama TFS na vikundi mbalimbali, vikiwemo vya kuzoa
taka” alisema Mfinanga.
Kilele
cha siku ya Mazingira Duniani huadhimishwa Juni 5 kila Mwaka na huambatana na
jumbe mbalimbali kama sehemu ya kueleimisha Jamii, ambapo kaulimbiu ya Mwaka
huu inasema “Mkaa ni gharama, tumia nishati mbadala”.
No comments:
Post a Comment