Mgombea aliyeshindwa nafasi ya Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Samwel Mziba (CHADEMA) akitoa neno kwa wajumbe mara baada ya matokeo kutangazwa kufuatia uchaguzi uliofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa hiyo. |
...............................................................................................
..............................................................
NAIBU
Meya wa Manispaa ya Dodoma aliyemaliza muda wake Jumanne Ngede amefanikiwa
kutetea nafasi yake katika uchaguzi uliofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa
ya Dodoma ambapo wajumbe 56 walishiriki uchaguzi huo.
Katika uchaguzi huo
Ngede ambaye ni Diwani wa Kata ya Chamwino kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 47 dhidi ya mpinzani wake kutoka Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Samwel Mziba ambaye ni Diwani wa Kata ya Hazina aliyepata
kura 9.
Mkurugenzi wa Manispaa
ya Dodoma ambaye ni Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Dodoma Mjini Godwin
Kunambi alimtangaza rasmi Ngede kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Dodoma.
Baada ya kufanikiwa
kutetea nafasi yake, Ngede aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua kwa kura nyingi
jambo linaonesha kuwa wana imani kubwa na utendaji wake na kwamba ataendelea
kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kwa kushirikiana na Madiwani wote.
Kwa upande wake, mgombea
aliyeshindwa Samweli Mziba aliwashukuru wajumbe na kumpongeza mshindi huku
akidai uchaguzi umepita na sasa ni kuchapa kazi tu.
No comments:
Post a Comment