Wednesday, March 29, 2017
MLYAMBATE Blog : TOVUTI ZA SERIKALI HEWANI RASMI: TOVUTI ZA SERIKALI KUBORESHA USIMAMIZI NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI Sekretarieti za mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Halmashauri zake 18...
Wednesday, March 8, 2017
AUSTRIA KUWEKEZA DODOMA
Naibu Meya wa Jiji la Linz Austria Detlef Wimmer (aliyesimama) akitoa hotuba yake |
Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Jaffar Mwanyemba akizungumza na Wanahabari kuhusu ushirikiano wa Manispaa hiyo na jiji la Linz la Austria |
|
Ziara katika shamba la zabibu |
Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Jaffar Mwanyemba na Naibu Meya wa jiji la Linz la Austria Detlef Wimmer wakisaini hati ya makubaliano ya mashirikiano. |
Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Jaffar Mwanyemba na Naibu Meya wa jiji la Linz la Austria Detlef Wimmer wakionesha hati ya makubaliano ya mashirikiano mara baada ya kusaini. |
Halmashauri
ya Manispaa ya Dodoma na jiji la Linz la nchini Austria zimesaini hati ya
makubaliano (Memorandum of Understanding) ya ushirikiano katika nyanja za Utunzaji
wa Mazingira, kuimarisha huduma za kijamii, uwekezaji wa kibiashara, kuimarisha
miundombinu na teknolojia, na kuimarisha huduma ya kupambana na majanga ya moto
na uokozi.
Maeneo
mengine ambayo mamlaka hizo mbili zimekubaliana kushirikiana ni pamoja kutoa
mafunzo mbalimbali wa watumishi wake na Madiwani wa pande zote mbili,
kubadilishana watumishi pamoja na kushirikiana katika jambo lolote litakaloonekana
kuwa na manufaa kwa wananchi wa pande zote.
Makubaliano
hayo yalifikiwa hivi karibuni wakati wa
ziara ya siku moja ya Naibu Meya
wa jiji la Linz Detlef Wimmer na ujumbe wake katika Manispaa ya Dodoma ambapo
alitembelea maeneo kadhaa ikiwemo Dampo la kisasa la takataka lililopo katika
kijiji cha Chidaya kata ya Ntyuka Manispaa ya Dodoma na shamba la zabibu katika
kata ya Mtumba ili kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo.
Akisaini
makubaliano hayo kwa niaba ya Manispaa ya Dodoma, Meya wa Manispaa hiyo
Mstahiki Jaffar Mwanyemba alisema ushirikiano huo umekuja wakati muafaka na
kwamba utakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa miji hiyo huku akitoa wito kwa marafiki
na wawekezaji wengine kujitokeza kwani
mji wa Dodoma kwa sasa umefunguka na kwamba ni wakati muafaka wa kuwekeza
Dodoma.
Kwa upande wake Naibu Meya wa jiji la Linz
Detlef Wimmer ambaye alisaini hati hiyo kwa niaba ya mamlaka ya jiji hilo
alielezea kuvutiwa kwake na mji wa Dodoma na kwamba amejifunza mengi katika
ziara yake huku akiahidi ushirikiano wa dhati katika maeneo waliyokubaliana.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi alisema ushirikiano kati ya Manispaa ya
Dodoma na Jiji la Linz ni mwanzo tu wa juhudi zinazofanywa na Manispaa katika
kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji
mbalimbali ili kuhakikisha Manispaa hiyo inakua kwa kasi huku huduma za kijamii
zikipewa kipaumbele kwa manufaa ya wakazi wake na hata wa mikoa ya jirani.
Thursday, December 22, 2016
Tuesday, December 6, 2016
LAPF 'YAIPIGA TAFU' MANISPAA YA DODOMA
![]() |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi |
MFUKO wa Pensheni wa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa
(LAPF) umekabidhi hundi ya Sh. 6 milioni kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
ili kutatua tatizo la uhaba wa maji katika maeneo ya Ihumwa na Mtumba ndani ya Manispaa hiyo.
Akikabidhi
hundi hiyo kwa Godwin Kunambi,
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma mjini humo, James Mlowe ambaye ni Meneja
Mawasiliano na Masoko wa LAPF amesema, mfuko huo umetoa kiasi hicho cha fedha
kwa ajili ya kufufua visima vya maji vilivyoharibika.
Amesema mfuko huo ulipokea maombi kutoka katika Ofisi ya
Manispaa pamoja na ofisi ya mbunge
kupatiwa msaada wa kutengeneza visima vya maji katika
Kata ya Ihumwa na Mtumba kutokana na visima hivyo kuharibika na kuwasababishia
usumbufu wa kukosea maji wakazi hao.
Amesema LAPF kama taasisi ya serikali, imekuwa ikifanya
shughuli nyingi na halmashauri mbalimbali nchini hususani shughuli za
maendeleo.
“Kwa sasa Dodoma ni Makao Mkuu ya Nchi hivyo kuna watu
wengi watahamia hivyo hakuna sababu ya kuwepo ukosefu wa maji.
“Kadri watu wanavyoongezeka ndivyo mahitaji
yanavyoongezeka hivyo mahitaji ya maji ni makubwa zaidi katika Mji wa Dodoma na
Ihumwa na Mtumba ni sehemu mahitaji hayo,” amesema Mlowe.
Hata hivyo Mlowe amesema, pesa zinazotolewa na taasisi
mbalimbali pamoja na wahisani ni vyema zikatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa
badala ya kuzibadilishia matumizi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amesema katika uongozi wake,
atahakikisha miradi yote iliyokusudiwa inafanyika.
“Ni kweli kwa sasa Dodoma kuna changamoto kubwa ya
ukosefu wa maji katika maeneo ambayo yapo nje ya mji".
“Msaada ambao tumeupata kutoka LAPF utasaidia kuboresha
na kukarabati visima vya maji ili wananchi waondokane na adha ya upatikanaji wa
maji,”alisema Kunambi.
KWA MSAADA WA MWANAHALISI ONLINE.com
Monday, November 7, 2016
Thursday, August 11, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)