Wajumbe wakifuatilia uwasilishaji wa Taarifa. |
Wajumbe waalikwa wakifuatilia uwasilishaji wa Taarifa. |
Wajumbe wakifuatilia uwasilishaji wa Taarifa. |
Baadhi ya Wataalamu wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifuatilia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Dodoma uliopokea taarifa ya Utekeleza wa Ilani ya CCM kuanzia 2015 hadi 2017. |
..................................................
HALMASHAURI ya Manispaa ya
Dodoma inatarajia kukusanya zaidi ya Shilingi bilioni 67.1 kutoka katika vyanzo
vyake vya ndani vya mapato katika mwaka ujao wa Fedha.
Kati ya Fedha hizo, zaidi
ya Shilingi bilioni 54.5 sawa na asilimia 81 zitaelekezwa kwenye miradi mbalimbali
ya maendeleo ya Wananchi.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
wa Manispaa hiyo Godwin Kunambi wakati ukiwasilisha taarifa ya Mikakati na
Mipango mbalimbali ya Maendeleo inayotarajiwa kutekelezwa na Manispaa hiyo
mbele ya Kamati ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya
Dodoma jana.
Kikao hicho kilichofanyika
katika Ofisi Kuu ya CCM Taifa Mjini Dodoma, kilikuwa maalum kwa ajili ya
wajumbe kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kuanzia mwaka 2015 hadi
2017, ambayo awali iliwasilishwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deo Ndejembi.
Akizungumza katika kikao
hicho, Mkurugenzi Kunambi aliwaambia wajumbe wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM
wa Wilaya hiyo Robert Mwinje kuwa, endapo Manispaa ya Dodoma itafanikiwa
kufikia lengo hilo la makusanyo, itakuwa ni Halmashauri ya pili Nchini Tanzania
kwa kukusanya Fedha nyingi kutoka katika vyanzo vya ndani ikitanguliwa na
Manispaa ya Ilala.
Alisema hatua hiyo
itaifanya Manispaa ya Dodoma kujiongezea uwezo mkubwa wa kujitegemea ikiwa ni
pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi zaidi.
Aliema kuwa, katika
kuimarisha ukusanyaji, baadhi ya mikakati itatiliwa mkazo zaidi ikiwemo matumizi
ya vifaa na mifumo ya Kielektroniki katika kukusanya, kuwa na takwimu sahihi,
usimamizi wa karibu kwa kila chanzo, uibuaji wa vyanzo vipya vya mapato, na kufanya
tathimini za mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment