Moja ya vifaa vya kutunzia taka kilichopo mkabala na Viwanja vya Nyerere katikati ya Mji. |
..................................................
HALMASHAURI ya Manispaa ya
Dodoma kupitia Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu imeendelea kuimarisha
miundombinu ya usafi kwa kuongeza vifaa vya kutunza uchafu katika mitaa kadhaa ya Mji ili
kuhakikisha Wananchi hawatupi taka ovyo wanapokuwa katika shughuli zao za kila siku.
Akizungumza wakati wa
uwekji wa vifaa hivyo, Mkuu wa Idara hiyo Dickson Kimaro alisema Manispaa inatarajia
kuongeza ‘vitunza uchafu’ 11 katika mitaa mbalimbali
ili kuweka mazingira rafiki ya kutunza uchafu kwa Wakazi wa Mji wanaokuwa
katika shughuli zao za kila siku.
“Hizi ni juhudi za makusudi
ili kuhakikisha Mji wetu unakuwa safi muda wote…natoa wito kwa Wakazi wa
Manispaa yetu watumie vifaa hivi kuhifadhia uchafu mdogo wanapokuwa katika
shughuli zao za kila siku” alisema Kimaro.
Alisema mbali na vifaa
hivyo, tayari Manispaa ilishasambaza vifaa vikubwa vya kukusanyia taka za aina
zote (Skip Bucket) 61 katika Kata mbalimbali zinazotumika kama vituo vya
kukusanyia taka kabla ya kubebwa na Mitambo ya Manispaa na kupelekwa katika
Dampo la Kisasa lililopo eneo la Chidaya Kata ya Matumbulu nje kidogo ya Mji.
No comments:
Post a Comment