............................................................
WAJUMBE wa Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Serikali za Mitaa ya Bunge la Uganda wameishukuru Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma kwa kuipatia Serikali ya Nchi hiyo kiwanja chenye ukubwa wa
eka tano katika Kata ya Mtumba eneo utakapojengwa Mji wa Serikali.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Reagan
Okumu alitoa Shukrani hizo jana wakati Kamati hiyo ilipotembelea Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma walipokuwa katika ziara ya siku moja ya kujifunza mambo
mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama Dampo la
kisasa la kuhifadhia taka kwa kuzifukia ardhini (Sanitary Land Fill) lililopo
Kata ya Matumbulu ambalo ni moja ya miradi mikubwa katika eneo la usafi na
utunzaji wa mazingira.
Awali akizungumza mbele ya
Kamati hiyo, Mhandisi wa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ambaye
alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Godwin Kunambi, aliwajulisha
wajumbe hao kuwa, Halmashauri imetenga na kupima eneo litakalojengwa Mji wa
Serikali hapa Dodoma na kwamba Serikali ya Uganda imepewa kiwanja chenye ukubwa
wa eka tano kwa ajili ya matumizi ya kiofisi, ambapo pia walioneshwa ramani ya eneo
hilo.
Wajumbe wa Kamati hiyo waliezea
kufurahishwa kwao na hatua hiyo huku wakiahidi kufikisha taarifa hizo njema kwa
Wananchi wa Uganda mara watakaporejea Nchini humo.
No comments:
Post a Comment