Baadhi ya Wazee wa Kata ya Mkonze Jijini Dodoma wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa utaoji wa vitambulisho vya Wazee uliofanywa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Selemani Jaffo leo Mei 26, 2018. |
...........................................................................
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani
Jaffo amesema, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ni ya mfano Nchini katika kuwatambua
na kuwatengenezea vitambulisho maalum vya kuwatambulisha Wazee katika maeneo ya
huduma mbalimbali ikwemo matibabu, akiwa ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya
Wazee ya mwaka 2003 inayolenga katika kuhakikisha kuwa, Wazee wa Tanzania
wanatambuliwa na wanapewa fursa ya kushiriki katika mambo yanayohusu maisha ya
kila siku na kupata huduma zote za msingi.
Waziri
Jaffo ameyasema hayo mapema leo Mei 26, 2018, alipokuwa akizindua rasmi zoezi
la utoaji wa vitambulisho vya Wazee kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Kata
ya Mkonze iliyopo umbali wa kilometa 4.7 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo ambayo pia
ilihudhuriwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deo Ndejembi na Mkurugenzi wa
Jiji hilo Godwin Kunambi, Waziri huyo aliagiza Halmashauri za Mikoa yote 26 ya Tanzania
Bara kuhakikisha zinawatambua Wazee katika
maeneo yao na kuwasilisha taarifa kamili ya kila Mkoa kuhusu Wazee katika Ofisi yake ifikapo Juni 30, mwka huu.
Awali,
akiwasilisha taarifa ya utekeleaji wa zoezi hilo kwa niaba ya Mkurugenzi wa
Jiji la Dodoma Godwin Kunambi, Mganga Mkuu wa Jiji hilo Hamadi Nyembea alisema
Halmashauri ilianza zoezi hilo kwa kuwatambua Wazee katika Kata zote 41 za Jiji
la Dodoma, na kwamba mpaka sasa jumla ya Wazee 15, 854 wameshatambuliwa kutoka
katika Kata 33, sawa na asilimia 80.5.
Alisema,
hatua iliyofuata ni kuwapiga picha Wazee waliotambuliwa na kuwatengenezea vitambulisho,
zoezi lililoanza rasmi mwezi Februari Mwaka huu, ambapo jumla ya Wazee 1,118 wameshapigwa
picha katika Kata za Mkonze, Mnadani, Uhuru, Madukani, Makole na Majengo na
kwamba kazi hiyo inaendelea katika Kata zilizobaki.
“Jumla
ya vitambulisho 564 vya Wazee vimeshakamilika na wahusika watakabidhiwa rasmi
leo kwa ajili ya kuanza kuvitumia” alisema Mganga Mkuu huyo wakati akiwasilisha
taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment