|
..........................................................................
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola ameanza ziara ya kikazi ya wiki
moja katika Manispaa ya Dodoma jana ambapo alitembelea Ofisi za Halmashauri na
kupokea taarifa ya hali ya Mazingira kwa ujumla iliyowasilishwa na Mkuu wa
Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu Dickson Kimaro.
Naibu Waziri pia alipata
taarifa kutoka kwa wataalam wa taasisi zingine ambazo ni wadau wa Mazingira
ikiwemo Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Idara ya
Madini, na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambao amefutana nao
katika ziara hiyo.
Katika siku ya kwanza ya
ziara yake hapo jana, Naibu Waziri Lugola alitembelea Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Dodoma na Chuo Kikuu cha Mtakatifu John ambapo alikagua mifumo ya usimamizi
wa taka ambapo kwa ujumla alikiri kuridhishwa jinsi taasisi hizo
zinavyozingatia matakwa ya Sheria na taratibu za kuhifadhi Mazingira, lakini
aliziagiza kuhakikisha takataka zinazoteketezwa kwa kuchomwa moto zinateketea
kwa kiwango kinachokubalika.
Ziara ya Naibu Waziri
inaendelea leo Ijumaa Mei 18, 2018 ambapo pamoja na maeneo mengine, atatembelea
na kukagua mifumo ya usimamizi wa taka katika machinjio ya Punda iliyopo eneo
la Kizota na inatarajiwa kumalizika Mei 25, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment