Sehemu ya Dampo iliyoanza kutumika |
Sehemu ya pili ya Dampo ambayo itatumika baada ya sehemu ya kwanza kujaa |
...................................................................
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola ameipongeza Halmashauri ya Manispaa
Dodoma kwa ujenzi wa Dampo la kisasa la kuhifadhia taka kwa teknolojia ya
kuzizika ardhini (Sanitary Land Fill) lililopo eneo la Chidaya Kata ya
Matumbulu katika Halmashauri hiyo.
Alitoa pongezi hizo jana
baada ya kufanya ziara katika Dampo hilo kwa lengo la kukagua mifumo ya
usimamizi wa Mazingira.
“Mfikishieni Mkurugenzi wa
Halmashauri salamu zangu…nimeridhika na uendeshaji wa Dampo hili na jinsi
mnavyozingatia na kusimamia usalama wa Mazingira” alisema Naibu Waziri huyo.
Alisema ni fahari kubwa kwa Halamshauri
ya Manispaa ya Dodoma kuwa na Miundombinu ya kisasa ya usafi na kutaka taka
zote zinazozalishwa ziondolewe na kupelekwa katika Dampo hilo ili kufiki
malengo ya mradi huo.
Dampo hilo lilianza kujengwa
mwaka 2010 na hadi linakamilika limegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 7.1
ambazo ni mkopo kutoka Benki ya Dunia kupitia Serikali Kuu ikiwa ni utekelezaji
wa mradi wa kuendeleza Miji ya Kimkakati Tanzania (TSCP) inayoratibiwa na Ofisi
ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Naibu Waziri Lugola alikuwa
katika siku ya pili ya ziara yake ya siku saba katika Wilaya ya Dodoma ambapo
pamoja na mambo mengine, anakagua jinsi mifumo ya usimamizi wa Mazingira katika
taasisi mbalimbali ikiwemo Hospitali na Vyuo inavyosimamiwa na kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment