Muhudumu wa Afya Ruth Azaliwa akimchoma Sindano ya chanjo dhidi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari ya Dodoma Huda Khalid Rabash kuashiria uzinduzi wa zoezi la utoaji wa chanjo hiyo katika Wilaya ya Dodoma jana. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deo Ndejembi (kushoto) na Mwalimu wa Afya wa Shule hiyo Caritas Burchard (kulia). |
Sehemu ya Wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Dodoma wakifuatilia shughuli ya uzinduzi wa utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi uliofanyika katika Shule hiyo jana. |
................................................
ZOEZI
la utoaji wa chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi
kwa Wanawake limezinduliwa rasmi katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma huku
wasichana waliopatiwa chanjo hiyo wakitoa wito kwa wenzao kujitokeza na
kuhakikisha wanakingwa dhidi ya ugonjwa huo.
Uzinduzi
huo umefanyika jana katika ukumbi wa Dodoma Sekondari ambapo mgeni rasmi katika
hafla fupi ya uzinduzi huo alikuwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deo Ndejembi
huku Mganga Mkuu wa Halmashauri Hamadi Nyembea akimwakilisha Mkurugenzi Godwin
Kunambi.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo, Kaimu Mkuu huyo wa Wilaya alisema uzinduzi huo ni
kiashiria cha kuwafikia Wasichana wote wenye chini ya umri wa miaka 14 ndani ya
Wilaya ya Dodoma.
Alisema
zoezi hilo litaendeshwa na Halmashauri kupitia Ofisi ya Mganga Mkuu, na
litashirikisha viongozi wa ngazi zote ikiwemo Kata na Mitaa ili kuhakikisha
kila msichana anayehusika anafikiwa na kupatiwa chanjo hiyo.
Awali,
Mganga Mkuu wa Halmashauri Hamadi Nyembea alisema katika kipindi cha Mwaka
mmoja ujao, jumla ya Wasichana 7,828 walio na umri wa chini ya miaka 14
wanatarajiwa kufikiwa na kupatiwa chanjo hiyo katika Wilaya ya Dodoma.
Alisema
baada ya miezi sita Wasichana wote
waliopatiwa chanjo hiyo watapatiwa tena kwa awamu ya pili ili kukamilisha kinga
yao dhidi ya virusi vinavyoeneza ugonjwa huo.
Alimweleza
Mgeni rasmi na wajumbe kuwa, chanjo hiyo imethibitishwa na Shirika la AfyaDuniani
(WHO) hivyo Wasichana na Wazazi wasiwe na mashaka badala yake watoe ushirikiano
wa kutosha ili kufikia lengo la Serikali la kutokomeza ugonjwa huo kama
ilivyofanya kwa magonjwa kama Polio.
No comments:
Post a Comment